Dk. Ali Akbar Salehi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma mkono wa rambirambi kwa viongozi na wananchi wa Nigeria kufuatia ajali mbaya ya ndege iliyopelekea watu 160 kupoteza maisha mjini Lagos.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk. Ali Akbar Salehi amemtumia ujumbe wa rambirambi waziri mwenzake wa Nigeria na kumuelezea masikitiko ya Tehran kufuatia ajali mbaya ya ndege iliyotokea siku ya Jumapili mjini Lagos ajali ambayo inahesabiwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Nigeria katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Juzi Jumapili, Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo alitangaza siku tatu za maombolezo na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu ajali hiyo.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Nigeria limesema kuwa, hakuna hata mtu mmoja aliyenusurika na kifo katika ajali ya ndege hiyo iliyokuwa inamilikiwa na shirika binafsi la Dana Air.

No comments:
Post a Comment