Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 17, 2012

Watu 8 wauawa na makumi kadhaa wajeruhiwa katika mripuko wa bomu nchini Iraq

Mripuko wa bomu la kutegwa uliotokea leo mjini Baghdad, Iraq umepelekea watu 8 kuuawa na makumi kadhaa ya wengine kujeruhiwa. Mripuko huo unakuja baada ya siku tatu tu ya mfululizo wa miripuko iliyotokea katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ambapo watu wapatao 70 waliuawa na wengine 200 kujeruhiwa. Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki amelaani vikali mauaji hayo na kuvitaka vikosi vya Iraq kupambana vikali na magaidi wasioitakia kheri nchi yake. Al Maliki amesisitiza kwa kusema kuwa, askari wa Iraq wanatakiwa kufanya kazi ya ziada katika kukabiliana na aina yoyote ya vitendo vya namna hiyo na kwamba, vitendo hivyo kamwe havitakiwi kushuhudiwa tena nchini humo.
Magaidi ambao wanapata misaada ya hali na mali kutoka nchi kadhaa za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia, siku za hivi karibuni wameshadidisha mashambulizi makali ya kigaidi, ili kwa njia hiyo wapate kuionyesha nchi hiyo kuwa haina usalama wa ndani.

No comments: