
Afrika Mashariki sasa imegeuka kuwa eneo la kistratijia la nishati baada ya kugunduliwa kiasi kikubwa cha gesi na mafuta huko Msumbuji, Tanzania, Uganda na Kenya.
Akizungumza mjini Washington, Diop amesema Tanzania ambayo ina uchumi wa pili kwa ukubwa Afrika Mashariki, inatazamiwa kushuhudia ongezeko la pato lake kwa dola bilioni tatu kwa mwaka kufuatia kugunduliwa akiba kubwa ya gesi katika pwani yake. Amesema fedha hizo ni nyingi sana na hivyo kunahitajika mipango ya mapema na kuanzishwa taasisi za kusimamia vizuri utajiri huo. Weledi wa mambo wanahofu kubwa kuwa, iwapo hautakuwepo usimamizi bora, huenda utajiri mpya wa gesi na mafuta Afrika Mashariki ukageuka kuwa laana kama inavyoshuhudiwa katika baadhi ya nchi za Afrika.
No comments:
Post a Comment