Makundi ya waasi yamekataa kusikiliza matakwa ya jamii ya kimataifa ya kutoa fursa ya kufanya kazi mpango wa Kofi Annan.
Huku juhudi za kila upande za kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria zikiendelea, magenge ya waasi yanayoungwa mkono na madola ya kigeni yamesema kuwa, hayatoheshimu mpango wa Kofi Annan, mpatanishi wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro huo.
Huku hayo yakiripotiwa, Russia na Umoja wa Ulaya zimesema kuwa zinaunga mkono mpango wa Kofi Annan na kusema kuwa hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria.
Rais Vladmir Putin wa Russia na mkuu wa Baraza la Ulaya jana usiku waliwaambia wandishi wa habari kuwa pande husika nchini Syria zinapaswa kuheshimu mpango wa vipengee sita wa Kofi Annan na kuashiria kuwa, wasioheshimu mpango huo hawana nia ya kuutatua mgogoro wa Syria.
Ingawa Umoja wa Ulaya umedai kuunga mkono mpango huo wa Kofi Annan, lakini pia umesema kuwa chaguo la nguvu za kijeshi liko mezani wakiwa na maana ya kutishia kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Syria.
Hata hivyo wataalamu mbalimbali wa mambo wamesema kuwa, ni jambo lililo mbali kwa Umoja wa Ulaya kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Syria hasa kwa vile nchi hiyo inapakana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Baadhi ya wachambuzi hao wa mambo wamesema kuwa, kuna hatari ya hata kutokea Vita vya Tatu vya Dunia kama Syria itavamiwa kijeshi.

No comments:
Post a Comment