Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, June 5, 2012

Uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia wa Bunge nchini Libya waakhirishwa

Maafisa wa Libya wametangaza kuwa uchaguzi wa bunge wa nchi hiyo umeakhirishwa hadi wiki ya kwanza ya mwezi ujao wa Julai. Uchaguzi huo utakaokuwa wa kwanza wa kidemokrasia tangu kupinduliwa utawala wa muda mrefu wa dikteta Muammar Gaddafi, hapo mwanzo ulikuwa umepangwa kufanyika Juni 19. Wabunge 200 wanatakiwa kuchaguliwa na kuchukua jukumu la kuandaa katiba ya Libya, lakini maafisa wa nchi hiyo wanasema kwamba wanahitajia muda zaidi ili kupitisha wagombea wanaostahili. Sghair Majeri Naibu Mkuu wa zamani wa Tume ya uchaguzi ya Libya aliacha kazi mwezi uliopita wa Mei na kusema kuwa hana uhakika matayarisho yatakuwa yamekamilika kwa kufanyika uchaguzi huo katika muda uliopangwa.
Zoezi la kuwapitisha wagombea wa uchaguzi huo wa bunge ambao idadi yao inakaribia 4,000 ilikuwa imepangwa kumalizika Juni 6.

No comments: