Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema kuwa, mazungumzo yake ya mjini Tehran na viongozi mbalimbali wa Iran yamekuwa mazuri na chanya.
Yukiya Amano aliwasili hapa mjini Tehran kwa ajili ya mazungumzo rasmi kuhusu shughuli za nyuklia za Iran.
Amesema, kuna baadhi ya mambo bado hayajajadiliwa lakini si masuala ambayo yanaweza kukwamisha mazungumzo.
Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA imefanyika hapa mjini Tehran katika wakati huu ambapo Iran inatarajiwa kufanya mazungumzo na kundi la 5+1 kuhusu shughuli zake za amani za nyuklia mjini Baghdad, Iraq.
Tayari Dk. Saeed Jalili, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameshawasili mjini Baghdad akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Iran kwa ajili ya mazungumzo hayo.Yukiya Amano aliwasili hapa mjini Tehran kwa ajili ya mazungumzo rasmi kuhusu shughuli za nyuklia za Iran.
Amesema, kuna baadhi ya mambo bado hayajajadiliwa lakini si masuala ambayo yanaweza kukwamisha mazungumzo.
Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA imefanyika hapa mjini Tehran katika wakati huu ambapo Iran inatarajiwa kufanya mazungumzo na kundi la 5+1 kuhusu shughuli zake za amani za nyuklia mjini Baghdad, Iraq.
Akiwa hapa mjini Tehran, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA ameonana na Dk. Jalili, pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran (AEOI) Bw. Fereydoun Abbasi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk. Ali Akbar Salehi.
No comments:
Post a Comment