Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 1, 2012

Watu 6 wauawa Somalia katika shambulizi la kujilipua kwa bomu

Watu wasiopungua sita wakiwemo wabunge wawili wameripotiwa kuuawa katika shambulizi la kujilipua kwa bomu lililofanyika leo katika mji wa Dhuusamareeb katikati mwa Somalia.
Muhammad Abdullah Muallim ambaye ni miongoni mwa viongozi wa kundi la Ahlusunna Waljamaa amesema shambulizi hilo la kujilipua kwa bomu limelenga hoteli moja ya mji huo na kuua watu kadhaa.
Mashahidi wa tukio hilo pia wamethibitisha kuwa wabunge wawili na raia wengine 4 wameuawa katika shambulizi hilo. Wamesema kuwa shambnulizi hilo lilitokea wakati wa chakula cha mchana na kwamba wabunge wengine wawili wamejeruhiwa. Wabunge hao walikuwa katika eneo hilo kuchunguza uwezekano wa kuanzisha idara ya masuala ya eneo hilo.
Dhuusamareeb ni mji wa kistratijia ulioko katika mkoa wa Galguduud na unadhibitiwa na kundi la Ahlusunna Waljamaa baada ya kuukomboa kutoka kwa wapiganaji wa kundi la al Shabaab.

No comments: