Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 1, 2012

Arab League: Saiful Islam ahukumiwe nchini Libya

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) imetangaza kwamba inaunga mkono azma ya Libya ya kumhukumu mwana wa dikteta aliyepinduliwa nchini humo Saiful Islam Gaddafi katika nchi hiyo. Katika taarifa yake jumuiya hiyo imesema, inaunga mkono kesi ya Saiful Islam kufanywa na vyombo vya mahakama vya Libya na kwamba serikali ya Tripoli imekariri mara kadhaa kuwa itahakikisha kesi hiyo inafanyika kwa uadilifu na bila upendeleo wowote.
Saiful Islam Gaddafi alitiwa nguvuni mwezi Novemba mwaka jana huko kaskazini mwa Libya na hivi sasa anashikiliwa katika mji wa Zintan, ulioko kilometa 180 kusini magharibi mwa mji mkuu, Tripoli.
Aprili 6 Libya ilipinga rasmi takwa la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) la kutaka mwana huyo wa Gaddafi akabidhiwe haraka kwa korti hiyo ya kimataifa ili ahukumiwe huko Uholanzi kutokana na makosa ya kutenda jinai dhidi ya binadamu.

No comments: