Waandamanaji 20 wameuawa katika maandamano nje ya jengo la wizara ya ulinzi mjini Cairo Misri.
Duru zinaarifu kuwa mauaji hayo yametekelezwa na genge lisilojulikana la watu wenye silaha. Wamisri wamekuwa wakiandamana nje ya jengo la wizara ya ulinzi mjini Cairo wakitaka utawala wa kijeshi uondoke madarakani.

Duru zinaarifu kuwa wanajeshi wametumwa katika eneo la kati kati mwa mji wa Cairo ili kuzia ghasia kuenea.
Wagombea wawili wa kiti cha urais wamesimamisha campeni zao kufuatia mauaji hayo. Mohammad Mursi wa Ikwanul Muslimin amesema amesitisha kampeni yake kwa masaa 48 kuonyesha 'mfungamano na waandamanaji'. Mgombea mwingine Abdel Moneim Abul Fotouh naye pia amesitisha kampeni zake.
Uchaguzi wa rais nchini Misri unatazamiwa kufanyika Mei 23 na 24 na baraza linalotawala la kijeshi limeahidi kukabidhi madaraka kwa mshindi mwezi Juni. Hatahivyo Wamisri wanasema wanajeshi wanapanga njama za kubakia madarakani.
No comments:
Post a Comment