Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 3, 2012

Watanzania wapata afueni, bei ya petroli na diseli yapungua

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania imetangaza kupungua kwa bei za Petroli na Diseli, jambo linaloonyesha kuwapo kwa unafuu kiasi fulani. Bei ya petroli imepungua kwa asilimia 2.16 sawa na shilingi 48 na dizeli kwa asilimia 2.59 sawa na shilingi 54 kuanzia leo Jumatano.
Mkurugezi wa mamlaka hiyo, Haruna Masebu amesema kuwa punguzo hilo limetokana na mabadiliko ya bidhaa hiyo katika soko la kimataifa na vilevile kupungua gharama za usafirishaji. Katika siku za huko nyuma, wananchi wengi wa Tanzania walikuwa wamelalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa hizo muhimu hususan kwa kuzingatia kuwa nchi hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nishati ya umeme.

No comments: