Takwimu zilizotolewa jana na Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba zaidi ya watu laki mbili na 40 elfu wamekimbia makazi yao huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya Disemba mwaka jana na Machi mwaka huu na kuifanya idadi ya wakimbizi nchini huyo kufikia milioni mbili tangu mwaka 2000.
Takwimu zilizotayarishwa na Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa zinasema kuwa idadi ya wakimbizi nchini Congo imeongezeka na kufikia milioni mbili hadi Machi mwaka huu.
Takwimu zilizotayarishwa na Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa zinasema kuwa idadi ya wakimbizi nchini Congo imeongezeka na kufikia milioni mbili hadi Machi mwaka huu.
Takwimu hizo zinasema kuwa majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Congo na yana karibu asilimia 70 ya wakimbizi milioni mbili wa nchi hiyo. Idadi hiyo inaendelea kuongezeka kutokana na mapigano makali yaliyoanza Jumapili iliyopita kati ya jeshi la serikali ya Kinshasa na makundi ya waasi. Mapigano hayo yamewalazimisha watu elfu tatu kukimbia makazi yao ambapo wengine wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda.
Hata hivyo takwimu za Umoja wa Mataifa zimeonesha kwamba idadi ya wakimbizi hao imepungua kiasi katika jimbo la Mashariki licha ya kuwepo hapo wapiganaji wa kundi la Kikristo la Lord's Resistance Army kutoka Uganda ambalo linahesabiwa kuwa miongoni mwa magenge ya kikatili zaidi ya uasi duniani.
No comments:
Post a Comment