Viongozi wa nchi za Magharibi mwa Afrika wanakutana leo katika mji mkuu wa Senegal, Dakar kwa shabaha ya kuchunguza migogoro ya Mali na Guinea Bissau.
Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) imesema kuwa viongozi wa nchi wanachama wanakutana leo katika kikao cha dharura mjini Dakar kwa ajili ya kuchunguza njia za kutatua migogoro ya Mali na Guinea Bissau.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa kikao hicho kitajadili hali ya mambo nchini Guinea Bissau baada ya kushindwa kufikiwa makubaliano baina ya Kundi la Mawasiliano la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa ECOWAS na viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo juu ya mipango ya kipindi cha mpito cha muda wa miezi 12 ikiwa ni pamoja na suala la kuteuliwa rais mpya wa nchi hiyo.
Mapinduzi ya kijeshi ya Guinea Bissau yaliyofanyika Aprili mwaka huu yalimuondoa madarakani rais wa zamani wa nchi Raimundo Pereira. Wanajeshi wa Mali pia walipindua serikali ya kiraia ya nchi hiyo mwezi Machi mwaka huu. Wakati huo huo hali ya mambo inaripotiwa kuwa si shwari mjini Bamako ambapo milio ya risasi inasikika huku na kule huku jeshi likiendelea kukabiliana na wanajeshi watiifu kwa rais aliyepinduliwa wa Mali Amadou Toumani Toure.
No comments:
Post a Comment