Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO limetetea hatua yake ya kuivamia kijeshi Libya na kudai kuwa lilijitahidi kadiri linavyoweza kukwepa kuua raia nchini Libya.
![]() |
Mji wa Sirte ulioharibiwa vibaya na mashambulizi ya kikatili ya NATO. Hivi sasa NATO wanadai walikuwa wakifanya mashambulizi kwa tahadhari kubwa huko Libya |
Msemaji wa NATO, Bi. Oana Lungescu amesema kuwa, wanasikitika sana kutokana na madhara yoyote ambayo huenda yakawa yamesababishwa na NATO wakati wa operesheni zake nchini Libya.
Amedai kuwa, si rahisi kukwepa madhara kikamilifu katika operesheni ya kijeshi.
Itakumbukwa kuwa ndege za NATO zilifanya jumla operesheni 26,500 yakiwemo mashambulizi 9,700 nchini Libya katika kipindi cha kuanzia Mwezi Machi hadi Oktoba 2011.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya, Mustafa Abdel Jalil, karibu watu 25,000 waliuawa na wengine 50,000 kujeruhiwa katika kampeni ya kumng'oa madarakani kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi kampeni ambayo ilianza mwezi Februari na kumalizika mwezi Oktoba 2011.
No comments:
Post a Comment