Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 15, 2012

Utawala wa Kizayuni wazidi kukosolewa Barani Ulaya kutokana na siasa zake za kujitanua

Umoja wa Ulaya umeukosoa vikali utawala haramu wa Israel kutokana na kile ulichokiita ni utawala huo kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina unazo zikalia kwa mabavu.
Mawaziri hao wa Mambo ya Nje wa Ulaya wameyasema hayo hii leo katika ripoti ya matamshi makali kwamba, utawala huo wa Israel unavunja mpango wa amani kwa kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi.

Ripoti hiyo aidha umeutaka utawala huo ghasibu kusimamisha mara moja ujenzi huo usio wa kisheria kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, sambamba na kubadilisha muamala mbaya unaoufanya utawala huo dhidi ya Wapalestina. Ripoti hiyo yenye kurasa tatu ya Mawaziri hao wa Umoja wa Ulaya imeongeza kuwa, ujenzi huo unapingana kabisa na sheria za Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo maandamano makubwa dhidi ya utawala haramu wa Israel yamefanyika katika nchi mbali mbali duniani kwa mnasaba wa kukumbuka tukio la kuanza kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na kuasisiwa utawala bandia wa Israel. Kwa upande wao Wapalestina wamesisitiza juu ya ulazima wa kurejea wakimbizi wa Kipalestina katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo bandia.

No comments: