SAKATA la wimbi la viongozi wa vyama vya siasa nchini kujiunga na Chadema, limeendelea mkoani hapa baada ya Makamu Mwenyekiti mstaafu wa TLP, Tanzania Bara, Westgate Rumambo kujiunga na chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati hivi karibuni, Rumambo alisema amejiunga Chadema baada ya kubaini ndicho chama pekee kinachotetea wanyonge.
“Jamani hivi sasa TLP haina mvuto tena, kwa wana mageuzi nchini kimeonekana ni chama cha mtu mmoja kuliko Chadema ambacho kina malengo mazuri ya kukomboa Watanzania hasa wa ngazi ya chini,” alisema Rumambo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati hivi karibuni, Rumambo alisema amejiunga Chadema baada ya kubaini ndicho chama pekee kinachotetea wanyonge.
Alisema atatumia uzoefu wake wa harakati za kuongoza mageuzi nchini, kuhamasisha jamii na kuiimarisha Chadema mkoani hapa, ili uhuru na mabadiliko ya kweli vipatikane.
Katibu Mwenezi wa Chadema Babati Mjini, Zahir Musa alisema wanampokea kwa mikono miwili Rumambo kwani ni mtu makini mwenye uchungu na mabadiliko.
Musa alisema watashirikiana na Rumambo katika uendelezaji wa Chadema mkoani hapa na wanatarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwake kwani ana uzoefu wa uongozi wa mageuzi nchini.
“Tumempokea mwanachama mpya wa Chadema na tunatarajia kumkabidhi kadi ya Chadema na kuanza mapambano ya kuhakikisha mwaka 2015 tunachukua jimbo la Babati Mjini,” alitamba Musa.
Rumambo hakukabidhi kadi yake ya TLP kwa madai kuwa ilishapotea muda mrefu na baadhi ya wafurukutwa wa Chadema mjini Babati walimpongeza kwa uamuzi wa kujiunga Chadema.
Walisema hivi sasa chama pekee cha upinzani kilicho na nia ya mabadiliko makini na chenye lengo la kuwafikisha wananchi wanakotaka ni Chadema pekee na ndiyo sababu vijana wengi wanaiunga mkono.
Walisema hivi sasa chama pekee cha upinzani kilicho na nia ya mabadiliko makini na chenye lengo la kuwafikisha wananchi wanakotaka ni Chadema pekee na ndiyo sababu vijana wengi wanaiunga mkono.
No comments:
Post a Comment