Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba, kuna haja ya kutekelezwa kikamilifu vipengee vyote vya mpango wa Kofi Annan mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria. Dakta Ali Larijani amebainisha kwamba, vipengee vyote vya mpango wa Kofi Annan kuhusu Syria vinapaswa kutekelezwa kikamilifu hasa katika suala la kuyapokonywa silaha makundi ya kigaidi. Amesema, makundi ya kigaidi ya Syria yanapaswa kutekeleza mpango wa Annan hasa kwa kutilia maanani kwamba, vikosi vya Syria vimehishimu mpango huo na kuondoka katika maeneo yaliyokuwa na mapigano. Spika wa Bunge la Iran ameashiria miamala ya kutilia shaka ya baadhi ya nchi za Kiarabu na Kimagharibi kuhusiana na matukio ya Syria na kusema kwamba, hali ya mambo inavyoelekea hivi sasa kuna matumaini ya kufanikiwa mpango wa Kofi Annan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment