Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 25, 2012

Assad: Mgogoro wa Syria umemalizika na kushukuru wananchi kwa kushikamana

Rais Bashar la Assad wa Syria amesema kwamba serikali yake imefanikiwa kukabiliana na mgogoro wa kisasa nchini humo pamoja na machafuko. Assad ameongeza kuwa Syria imeweza kukabiliana na mashinikizo na vitisho dhidi yake na kwamba hilo limefanikiwa kutokana na wananchi kusimama kidete pamoja na mshikamano wao. Katika upande mwingine Bunge jipya la Syria limefanya kikao chake cha kwanza mwaka huu wa 2012 katika mji mkuu wa nchi hiyo Damascus. Katika kikao hicho wabunge 250 waliapishwa kulitumikia taifa na kumchagua Muhammad Jihad al Lahham kuwa Spika wa Bunge. Wabunge 210 miongoni mwao ni wapya, asilimia 20 kati yao ni wanawake na kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kadhaa wabunge hao wa Syria wanatoka katika vyama tofauti, mrengo wa upinzani pamoja na shaksia wa kujitegemea.

No comments: