Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, April 23, 2012

Rais al Bashir wa Sudan: Hakuna tena mazungumzo na Sudan Kusini

Omar Al Bashir
Rais Omar al Bashir wa Sudan amesema kwamba hakutakuwepo tena mazungumzo kati ya nchi yake na Sudan Kusini. Al Bashir amesema hayo leo alipolitembelea eneo lenye utajiri wa mafuta la Heglig ambalo kwa siku kadhaa lilivamiwa na kukaliwa kwa mabavu na vikosi vya Sudan Kusini. Al Bashir ameongeza kwamba, hatafanya mazungumzo na viongozi wa Juba kwani wameonesha kuwa wanaweza tu kuelewa lugha ya mtutu wa bunduki. Al Bashir aliyewasili katika eneo la Heglig huku akiwa amevalia sare za kijeshi aidha ametishia kwamba, Sudan itawafunza somo Sudan Kusini ambalo hawatalisahau. Mgogoro kati ya nchi hizo mbili ulipamba moto baada ya Sudan Kusini kuvamia eneo muhimu lenye utajiri wa mafuta la Heglig, lililoko kusini mwa Sudan. Hatua hiyo ilikosolowa na Umoja wa Afrika na taasisi nyingine za kimataifa na kuongezwa uwezekano wa kuzuka vita kati ya pande mbili.

No comments: