Chama cha upinzani cha Nigeria cha Congress for Progressive Change (CPC) kimeahidi kuwa iwapo kitashinda uchaguzi ujao kitaunda serikali ya kidemokrasia, uadilifu na usawa nchini humo.
Msemaji wa chama hicho Rotimi Fashakin amesema kuwa viongozi wa chama hicho wanafanya jitihada za kuasisi harakati ya kisiasa yenye uwezo wa kuanzisha thamani za demkorasia halisi nchini humo.
Kushindwa kwa mwakilishi wa chama hicho cha CPC Muhammadu Buhari katika uchaguzi uliopita wa rais kulizusha machafuko na mapigano makali katika maeneo mbalimbali ya Nigeria. Katika uchaguzi huo Buhari alipata asilimia 32 ya kura na kushindwa na mpinzani wake Goodluck Jonathan. Wakati huo Kamisheni ya Uchaguzi ya Nigeria ilitangaza kuwa Jonathan ameshinda uchaguzi wa rais kwa kupata asilimia 59. Kambi ya upinzani ilikataa matokeo hayo na kudai kwamba kulifanyika udanganyifu na wizi wa kura.
Muhammadu Buhari anatambuliwa na Wanigeria wengi kuwa ni kiongozi safi asiyekuwa na doa na baadhi yao wanamwita Nelson Mandela wa Nigeria. Buhari ana historia ya kuwa mwanajeshi lakini alijiunga na chama cha CPC baada ya kustaafu jeshini. Upinzani wake mkubwa na pia chama chake dhidi ya udhibiti wa nchi za Magharibi nchini Nigeria na vita vya kupambana na ufisadi nchini humo vilitatiza mno uwezekano wa kushinda uchaguzi uliopita wa rais. Kwani madola ya Kimagharibi na mafisadi wakubwa katika serikali ya Nigeria walimtambua kuwa kikwazo na kizuizi cha maslahi yao.
Kushindwa kwa chama cha Congress for Progressive Change katika uchaguzi uliopita wa rais kuliambatana na machafuko na maandamano makubwa. Mapigano hayo yalikuwa makubwa kiasi kwamba jeshi la Nigeria lilitishia kuwa litashirikiana na polisi katika kukabiliana na wapinzani. Hata hivyo machafuko ya ndani ya Nigeria yaliendelea kuathiri hali ya kisiasa ya nchi hiyo.
Wafuasi wa chama cha CPC wanasema kwa mujibu wa matokeo ya kura za uchaguzi uliopita wa rais Goodluck Jonathan alipata asilimia 100 katika baadhi ya vituo vya kupigia kura vya kusini mwa Nigeria, suala ambalo wanasema ni muhali kutokea. Watu wengi waliuawa katika machafuko ya ndani ya baada ya uchaguzi wa Nigeria na maelfu ya wengine kuwa wakimbizi.
Mchafuko hayo ya kisiasa ya Nigeria sasa yanashika sura ya kikaumu na kidini suala ambalo linatishia mno usalama wa nchi hiyo kubwa ya Kiafrika.

No comments:
Post a Comment