Wanajeshi wa kulinda amani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wako Darfur
nchini Sudan wakihudumu katika fremu ya Kikosi cha Kulinda amani cha
Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, Kamanda wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Ataollah Salehi amesema Umoja wa Mataifa umetoa mafunzo maalumu kwa vikosi vya kulinda amani vya Iran. Mwaka 1992, Jeshi la Iran lilianzisha kikosi maalumu cha kulinda amani ambacho hutumwa kutoa huduma za kibinaadamu kote duniani. Wanajeshi wa kulinda amani wa Iran tayari wameshahudumu huko Sudan Kusini na pia walihududumu katika Pembe ya Afrika mwaka 2003 kufuatia mgogoro mkali wa mpakani kati ya Ethiopia na Eritrea. Hivi sasa kikosi cha kulinda amani cha Iran kiko Darfur magharibi mwa Sudan kwa lengo la kusaidia Umoja wa Mataifa kudumisha amani katika eneo hilo.
Kamanda ya Kikosi cha Nchi Kavu cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Ahmad-Reza Pourdastan amesema Iran iko tayari kutuma vikosi vyake vya kulinda amani eneo lolote duniani endapo Umoja wa Mataifa utawasilisha maombi yake.

No comments:
Post a Comment