Watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi nchini Mali huku mtoto mdogo
akiuawa kwa mripuko wa bomu kaskazini mwa nchi hiyo, hali inayoashiria
kuwepo mchafukoge katika eneo ambalo linadhibitiwa kwa muda wa wiki tatu
sasa na watu wenye silaha nchini humo. Aidha walioshuhudia tukio hilo
wamesema kuwa, kuna uwezekano mauaji hayo yamefanywa na wezi ambao
wanapatikana kwa wingi katika maeneo ya waasi wa Tuareg.
Waasi hao waliyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 22 mwezi uliopita mwaka huu.
Waasi hao waliyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 22 mwezi uliopita mwaka huu.
No comments:
Post a Comment