Bunge la Misri limepiga marufuku kugombea katika uchaguzi ujao wa rais watu waliokuwa karibu na Hosni Mubarak dikteta wa zamani wa nchi hiyo. Wawakilishi wa bunge la Misri wamefikia makubaliano kuhusu mpango huo unaowazuia watu wote waliokuwa karibu na Hosni Mubarak kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo kutoka Misri uamuzi huo wa wabunge wa Misri umechukuliwa baada ya Omar Suleiman mkuu wa zamani wa vyombo vya ujasusi vya Misri wakati wa utawala wa dikteta Hosni Mubarak kutangaza kuwa atagombea kiti cha urais katia uchaguzi ujao. Mpango huo wa kupiga marufuku maswahiba wa Mubarak kugombea katika uchaguzi ujao wa rais umepitishwa kutokana na kuweko wabunge wengi wanaoiunga mkono harakati ya Ikhwanul Muslimin katika bunge la Misri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment