Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa, Wamagharibi wameanza
kubadili misimamo kuhusiana na nchi yake baada ya kuelewa hatari
zinazoweza kuwakumba kutokana na hatua yao ya kuwaunga mkono magaidi.
Kiongozi huyo ameliambia gazeti la al-Akhbar la nchini Lebanon kuwa,
viongozi wa sasa na wale wa zamani wa Marekani wamekuwa wakijaribu
kuwasiliana na serikali yake lakini kutokana na lobi zinazowasukuma huko
Washington, wameshindwa kueleza bayana wanachokitaka.
Matamshi ya Rais
Assad yametolewa katika hali ambayo, viongozi wa kundi la G7
wamekubaliana kuweka mikakati ya kiusalama katika nchi zao ili
kukabiliana na tishio la magaidi wanaotoka nchini Syria.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa, wapiganaji wengi kwenye makundi ya
kigaidi huko Syria ni raia kutoka nchi za Ulaya. Ufaransa wiki iliyopita
ilitoa takwimu zinazoonyesha kuwa, kuna Wafaransa zaidi ya 900
wanaoshirikiana na makundi ya kigaidi nchini Syria. Wakati huo huo Rais
Bashar Asad amesema kamwe hatofanya mazungumzo na wapinzani wake
waishio nje ya nchi na kusisitiza kuwa, mazungumzo pekee
yatakayokubalika ni yale yatakayofanyika ndani ya ardhi ya Syria. Kuhusu
uchaguzi uliopita wa rais kiongozi huyo amesema kuwa, Wasyria
walizungumza kwa sauti kubwa na kuonyesha msimamo wao. Amesema jamii ya
kimataifa inafaa iheshimu maamuzi ya Wasyria.
No comments:
Post a Comment