Dakta Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani
Bunge amesema kuwa, kuna ulazima wa kuendelezwa mapambano dhidi ya
magaidi nchini Syria. Akizungumza kwenye kikao cha pili cha nchi
marafiki wa Syria kilichofunguliwa leo mjini Tehran, Dakta Larijani
ameongeza kuwa nchi za Magharibi zilifikiri kwamba, kwa kuvuruga amani
na utulivu nchini Syria zingeweza kuunusuru utawala wa Kizayuni wa
Israel.
Akielezea uchaguzi wa rais ulioanza kufanyika nje ya nchi hiyo
hivi karibuni, Dakta Larijani amesema kuwa, uchaguzi huo unathibitisha
kwamba serikali ya Syria inafuata na kuheshimu maamuzi ya wananchi.
Wakati huohuo, Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni
wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuongezeka idadi
ya nchi zinazoiunga mkono Syria kwenye mapambano dhidi ya makundi ya
kigaidi, ni ishara tosha kwamba walimwengu wanahitaji amani na utulivu
nchini humo. Alauddin Bourujerdi ameeleza kusikitishwa na uamuzi wa
Marekani wa kutuma silaha za kisasa nchini Syria na kutoa mafunzo kwa
magaidi hao na kusisitiza kwamba, jambo la kutia moyo ni kuona kwamba
siku hadi siku zinaongezeka nchi zinazoiunga mkono serikali ya Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment