Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika linakusudia
kujadili suala la kurudishiwa tena Misri uanachama katika jumuiya hiyo.
Ismail al Sharqi kamishna wa baraza hilo amesema kuwa, baada ya
kufanyika uchaguzi wa rais wa Misri wiki iliyopita, AU tarehe 25 Juni
itafanya kikao cha kujadili juu ya kuondoa marufuku iliyowekewa Cairo
katika umoja huo na kurejeshewa tena uanachama wake.
Baada ya jeshi kumpindua Muhammad Musri rais halali wa Misri
aliyechaguliwa na wananchi Julai mwaka jana, Umoja wa Afrika
ulisimamisha uanachama wa Cairo katika jumuiya hiyo. Uchaguzi wa rais
uliofanyika hivi karibuni ulisusiwa na mirengo mingi ya kisiasa huku
watu wachache tu wakishiriki kwenye zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment