Mamia ya wakimbizi wa Libya wamekataa kuondoka kwenye kambi ya
Choucha iliyoko kusini mwa Tunisia, licha ya jitihada za Kamisheni Kuu
ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa (UNHCR) ya kutaka kuifunga kambi hiyo.
Wakimbizi wa Libya wanaoishi katika kambi hiyo jana walikwamisha juhudi
za vikosi vya usalama vya Tunisia vya kutaka kuondoa mahema yao kambini
humo. Kambi hiyo ya Tunisia iliyoanzishwa mapema mwaka juzi hivi sasa
inawahifadhi mamia ya raia wa Libya waliokimbia machafuko yaliyopelekea
kung'olewa madarakani kiongozi wa nchi yao Kanali Muammar Gaddafi.
UNHCR ilitangaza mwezi Machi mwaka huu uamuzi wake wa kufunga kambi
ya Choucha ifikapo Juni 30. Hii ni katika hali ambayo Kamisheni Kuu ya
Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa jana pia ilisitisha misaada yake ya
kibinadamu yakiwemo maji, chakula, vifaa vya umeme na huduma za kitiba
kwa wkaimbizi wa kambi hiyo.
No comments:
Post a Comment