Ajali mbaya ya barabarani imesababisha vifo vya watu 18 katika eneo la Jinja, katikati mwa Uganda.
Habari zinasema kuwa lori moja lililokuwa limesheheni watu lilipinduka katika barabara kuu ya Jinja kuelekea Kamuli na kusababisha maafa hayo. Watu wengine 24 wamenusurika wakiwa na majeraja. Manusura wamewaambia waandishi wa habari kwmba dereva wa lori hilo ambaye pia amefariki dunia alikuwa mlevi na kwamba lori hilo lilikuwa likienda kwa mwendo wa kasi mno. Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu laki 10, 000 hufariki dunia kila mwaka nchini Uganda kutokana na ajali za barabarani. Wakati huo huo zaidi ya maspika 100 kutoka mabunge mbalimbali duniani wamekubali kujadiliwa kadhia ya Syria katika mkutano wa 126 wa mabunge ya dunia IPU unaondelea mjini Kampala, Uganda.
No comments:
Post a Comment