Waziri Mkuu wa Mpito nchini Mali ameunda serikali mpya nchini humo. Habari zinasema kuwa, Waziri Mkuu Cheick Modibo Diarra ametangaza serikali hiyo mpya inayoundwa na mawaziri 24 kupitia televisheni ya taifa ya nchi hiyo. Aidha serikali hiyo mpya haikujumuisha waziri yeyote wa serikali ya zamani. Tarehe 22 mwezi Machi mwaka huu jeshi la nchi hiyo lilimg'oa madarakani Rais wa nchi hiyo Amadou Toumani Toure na kutwaa madaraka ya uongozi kwa mabavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment