Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa kuboreka kwa uchumi wa
Zimbabwe kunaipa nchi hiyo fursa ya kusonga mbele iwapo tu chaguzi
zijazo nchini zitakuwa huru na za kiuadilifu. Obama amesema uchumi wa
Zimbabwe unaanza kuimarika kwa hiyo nchi hiyo ina fursa ya kupiga hatua
mbele za kimaendeleo. Rais wa Marekani aliyasema hayo jana katika hotuba
yake kwa njia ya televisheni katika Chuo Kikuu cha Cape Town nchini
Afrika Kusini.
Ameongeza kuwa Wazimbabwe wanaweza kujiainishia
mustakbali wao bila ya kuhofia vitisho na kuadhibiwa. Rais Obama amekuwa
ziarani barani Afrika ambapo hadi sasa tayari amekwishazitembelea
Senegal na Afrika Kusini na mchana huu anatazamiwa kuwasili Nchini
Tanzania kwa ziara ya siku mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment