Ismail Haniya Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina amesisitiza kuwa, baadhi ya nchi za Kiarabu zinashiriki katika njama zinazofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. Haniya amesema kwamba, baadhi ya nchi za Kiarabu zinashirikiana na Marekani na Israel katika njama za kuwauawa taratibu Wapalestina wa Gaza.
Aidha amesema utawala wa Kizayuni ndio unaobeba dhima kuhusiana na janga kubwa la kibinadamu linaloikumba Gaza kwa sababu ya kuendelea kuuzingira ukanda huo tokea ardhini, baharini na angani. Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina pia amesisitiza kuwa, serikali za Kiarabu zisizosema chochote kuhusu jinai za Israel, mzingiro wa Gaza na kuuawa polepole wakazi wa eneo hilo zisidhani kwamba zinachukuliwa na Wapalestina kuwa hazina hatia. Mzingiro wa kila upande wa Israel dhidi ya Gaza ulioanza mwaka 2007, umepelekea jumla ya wakaazi milioni moja na nusu wa eneo hilo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa bidhaa muhimu na mahitaji ya dharura kama vile chakula, maji safi ya kunywa, mavazi na madawa. Vilevile kukatwa mara kwa mara umeme na kwa muda mrefu kumezidisha matatizo na kuifanya hali ya kibinadamu ya eneo hilo izidi kuwa mbaya. Ijapokuwa Israel ililazimika kurejea nyuma kutoka Gaza mwaka 2005 baada ya kushindwa mara kadhaa na mapambano ya wananchi wa Palestina, lakini imekuwa ikizusha waziwasi ili kufidia kushindwa kwake na wakati huo huo kuandaa mazingira ya kuwafanya Wapalestina wasalimu amri na kukalia tena kwa mabavu Ukanda wa Gaza. Vilevile hata baada ya kuondoka huko Gaza si tu kwamba siasa za kiadui za Israel dhidi ya wakaazi wa Gaza hazikupungua, bali kivitendo hatua zisizo za kibinadamu za utawala huo ghasibu dhidi ya wakazi wa eneo hilo zimekluwa zikiendelea kama ilivyo katika maeneo mengine ya Palestina. Vitendo visivyo vya kibinadamu vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina havikomei tu katika mashambulizi ya kinyama dhidi yao, Israel pia inakusudia kuwaua Wapalestina kwa njia tofauti kama vile kuyazingira maeneo yao hasa Ukanda wa Gaza. Mzingiro wa kila upande wa Gaza na kutoruhusu Israel kuingizwa bidhaa muhimu na za dharura katika eneo hilo, kumezidisha shida na mateso kwa wakazi wa Gaza.
Katika miaka ya hivi karibuni, mamia ya Wapalestina wamepoteza maisha yao kutokana na matatizo yanayosababishwa na mzingiro huo. Ni wazi kuwa utawala wa Kizayuni unadumisha mzingiro wa Gaza kwa lengo la kuwaua polepole Wapalestina wanaoishi kwenye eneo hilo. Kuchelewa taasisi za kimataifa hasa Umoja wa Mataifa katika kuchukua hatua zinazotakiwa dhidi ya utawala huo pia kumeipa fursa zaidi Israel ya kuzidisha jinai zake dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina. Vilevile kimya cha madola ya Kiarabu mkabala na jinai za Israel, na kushiriki baadhi yao katika njama za Wamagharibi na Tel Aviv dhidi ya Wapalestina kunazifanya nchi hizo zionekane kama washirika wa jinai hizo za Wazayuni, ukweli ambao umebainishwa pia na Ismail Haniya. Kuchelewa taasisi za kimataifa hasa Umoja wa Mataifa katika kuchukua hatua zinazotakiwa dhidi ya utawala huo pia kumeipa fursa zaidi Israel ya kuzidisha jinai zake dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina. Vilevile kimya cha madola ya Kiarabu mkabala na jinai za Israel, na kushiriki baadhi yao katika njama za Wamagharibi na Tel Aviv dhidi ya Wapalestina kunazifanya nchi hizo zionekane kama washirika wa jinai hizo za Wazayuni, ukweli ambao umebainishwa pia na Ismail Haniya.

No comments:
Post a Comment