Watu wasiopungua saba wameuawa katika ghasia kati ya wafuasi na
wapinzani wa Rais Muhammad Mursi wa Misri. Hayo yameelezwa na duru za
usalama na kitiba za nchi hiyo. Watu watano waliuawa jana katika miji ya
kusini mwa Cairo, mmoja katika mji wa Beni Suef na mwingine huko
Fayoum. Duru za kitiba za huko Misri zimeripoti pia kuwa watu wengine
wawili walipoteza maisha wakati kulipozuka ghasia nje ya makao makuu ya
Ikhwanul Muslimin katika mji mkuu Cairo. Watu zaidi ya 600 pia
walijeruhiwa katika ghasia za jana.
Hayo yameripotiwa na Wizara ya Afya
ya Misri. Maandamano ya jana ya kumpinga rais wa Misri yametajwa kuwa
maandamano makuwba zaidi kuwahi kufanyika nchini humo katika historia ya
nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment