Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah Nabil Qawuq amesema kuwa, kamwe Hizbullah haitashirikiana na nchi za Marekani, Ufaransa na Uingereza dhidi ya Syria kwa kuwa, kama utawala wa Damascus utapata pigo, basi utawala pekee utakaonufaika ni utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika nchi za eneo hili. Akiashiria kupungua hali ya machafuko ndani ya nchi hiyo amesema, matarajio ya mabeberu ya kuung'oa utawala wa Syria yamepeperushwa na upepo na kwamba kwa kusimama kidete Syria, nchi hiyo imeweza kuvuka hatua ngumu zaidi na kuukatisha tamaa utawala wa Kizayuni.
Qawuq ameelezea kusikitishwa kwake na njama za Waarabu dhidi ya serikali ya Damascus na kusema kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu zinatumia pesa za mafuta yao kwa ajili ya kuunufaisha utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani.
Wakati huo huo, Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati hiyo Sayyid Hashem Safiyyudin amesema, pamoja na Muqawama wa Lebanon kukabiliwa na hali ya hatari ya njama za ndani na nje za maadui, lakini bado uko imara.

No comments:
Post a Comment