Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ali Akbar
Salehi amekutana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mjini Harare ambapo
wamefanya mazungumzo kuhusu njia za kustawisha uhusiano wa pande mbili.
Katika mkutano huo, Salehi amemkabidhi Mugabe salamu za Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na
rais-mteule Hassan Rohani. Kwa upande wake Rais Mugabe ameashiria safari
zake nchini Iran na kusema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
pia aliwahi kutembelea Zimbabwe wakati akiwa rais.
Mapema Waziri wa
Mambo ya Nje wa Iran alikutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa
Zimbabwe Simbarashe Mumbengegwi ampabo wawili hao wamepongeza uhusiano
baina ya nchi zao.
Katika mkutano huo Salehi alisema Iran na Zimbabwe ziko katika
mashinikizo na vikwazo haramu na hivyo nchi hizi mbili zinapaswa kuwa na
ubunifu katika kukabiliana na mzingoro wa maadui. Naye Mumbengegwi
alisema Iran, kama mwenyekiti wa mzunguko wa Harakati ya Nchi
Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM imeinua itibari ya
harakati hiyo. Aidha amepongeza misimamo imara ya Iran na Zimbabwe
pamoja na kuwepo mashinikizo ya kila aina dhidi yao.
No comments:
Post a Comment