Ralph Schoenman mchambuzi wa masuala ya kisiasa kimataifa amesema
kuwa wimbi la mashambulizi linaloendelea dhidi ya kanali za matangazo
za Iran ni kampeni inayotekelezwa na Washington ili kuandaa uwanja wa
kuvamiwa kijeshi Iran. Schoenman amesema kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya
ubeberu wa Marekani wa kutaka kuanzisha anga ya vita na Iran. Ameongeza
kuwa kitendo cha kufungia matangazo ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran, IRIB ni jaribio lenye lengo la kuwatisha wananchi
wa Iran na kuwazuia walimwengu kusikiliza maoni na mitazamo inayotolewa
na nchi zote zilizo chini ya mashambulizi na zile zinazolengwa na
ubeberu wa Marekani.
Mashirika kadhaa ya huduma za satalaiti duniani yakiwemo ya Eutelsat
na Intelsat yamesimamisha kurusha matangazo ya kanali kadhaa za Iran.
Intelsat ilisema Juni 19 mwaka huu kuwa haitatoa tena huduma kwa kanali
za Iran ikiwemo televisheni ya Press kuanzia leo Julai Mosi.
No comments:
Post a Comment