Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa Benjamin Netanyahu Waziri
Mkuu wa utawala wa Kizayuni amekataa masharti ya Wapalestina kwa ajili
ya kufanya mazungumzo. Wapalestina wanaitaka Israel isimamishe ujenzi
haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi na iwaachie huru wafungwa
wa Kipalestina kama sharti la kufanya mazungumzo na Tel Aviv.
Akizungumza hivi karibuni na waziri wa ngazi ya juu wa Israel,
Netanyahu
alisema kuwa hana nia ya kutangaza kusimamisha ujenzi wa vitongoji vya
walowezi wa Kiyahudi huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan au
kuwaachia huru wafungwa wa Kipalestina kama sharti la kuanza mazungumzo
kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Tel Aviv. Waziri
huyo wa ngazi ya juu wa utawala wa Kizayuni amesema Benjamin Netanyahu
amekataa masharti hayo ya Wapalestina na kwamba anataka kuanza
mazungumzo hayo bila ya masharti yoyote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment