Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya
Nje wa Russia amesema kuwa wapinzani wa Syria wanaoungwa mkono na nchi
za kigeni hawapaswi kuruhusiwa kuweka masharti ili kushiriki kwenye
mkutano wa pili wa Geneva. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa
suala la kutaka kumuondoa madarakani Rais Bashar Assad wa Syria
halipasi kuwa sharti la wapinzani la kushiriki kwenye mazungumzo hayo ya
amani.
Marekani na Russia zilikubaliana Mei 7
mwaka huu huko Moscow kuendesha mkutano wa kimataifa kuhusu Syria, ambao
utaufuatia ule wa awali uliofanyika mjini Gevena mwezi Juni mwaka jana.
Muungano wa upinzani wa Syria mwezi Mei mwaka huu ulieleza kuwa
hautashiriki mkutano wa pili wa Geneva iwapo haitaainishwa tarehe ya
kumlazimisha Rais Bashar Assad kujiuzulu kama njia ya kutatua mgogoro wa
nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment