Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran ipo tayari kutafuta ufumbuzi wa
matatizo ya kieneo. Ali Akbar Salehi amesema kuhusu uamuzi wa Cairo wa
kukata uhusiano wake na Syria kuwa, Misri ingeweza kuwa na nafasi kubwa
katika kutafuta suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo. Kuhusu matuiko ya
Bahrain, Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, masuala ya
Manama yanapaswa kutatuliwa na wananchi na serikali yenyewe na kwamba
Tehran inaamini kuwa uingiliaji wowote nchini humo hauna faida.
Ali Akbar Salehi pia amesisitiza juu ya
nafasi ya Iran katika kutatua migogoro ya kieneo na kuongeza kuwa
uchaguzi wa rais wa hivi karibuni hapa nchini utaboresha uhusiano kati
ya Iran na Magharibi.
No comments:
Post a Comment