Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amekaribisha makubaliano ya
amani yaliyotiwa saini kati ya serikali ya Mali na waasi wa Tuareg hapo
jana. Ban amesema pande mbili hizo zinafaa kuhakikisha kwamba
makubaliano hayo yanatekelezwa kikamilifu. Katibu Mkuu wa UN amesema
makubaliano hayo yataandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi mkuu wa rais
kwa njia ya amani na ameyataka makundi mengine ya waasi kufuata mfano
huo ili Mali iweze kurudi katika hali yake ya zamani ya uthabiti na
utulivu.
Ban Ki moon pia amewashukuru marais Blaise Compaoré wa Burkina Faso na Goodluck Jonathan wa Nigeria kwa juhudi zao za kuleta amani nchini Mali. Hapo jana, serikali ya Mali ilitiliana saini makubaliano ya amani na waasi wa Tuareg wanaopigania kujitenga eneo la Azawad, kaskazini mwa Mali na hivyo kuvifungulia njia vikosi vya serikali kurejea katika mji wa Kidal kabla ya kufanyika chaguzi mkuu mwezi Julai mwaka huu.

No comments:
Post a Comment