Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, June 14, 2013

UN yatoa ripoti ya Maendeleo kwa Lugha ya Kiswahili

Toleo la muhtasari wa ripoti ya maendeleo ya binadamu duniani imezinduliwa siku ya Jumatano katika Chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya. Hii ni mara ya kwanza ripoti hii imechapishwa kwa lugha ya Kiswahili.
Akizindua ripoti hiyo ya mwaka 2013, msimamizi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Kenya  Steven Ursino alisema  kuweko kwa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kwa lugha ya Kiswahili kutawasaidia wananchi kufahamu changamoto za maendeleo na kuwapa nafasi ya kutoa mchango wao ili kutatua matatizo yanayowakabili.
Naye Khalid Malik, mkurugenzi wa ofisi ya UNDP ya Ripoti ya Maendeleo amesema madhumuni ya ripoti ya maendeleo ya binadamu ni kuhusu kupanua uwezo wa binadamu kujiendeleza. Amesema ni muhimu kwamba ripoti hii imechapishwa kwa lugha ambazo watu wanaelewa kwa urahisi. Kwa mujibu wa ripoti hiyo nchi za Afrika Mashariki bado ziko nyuma katika maendeleo ya mwanaadamu. Kenya imechukua nafasi bora zaidi ya majirani zake ikiwa ya 145 kati ya nchi 187 duniani ikifuatiwa na Tanzania iliyoshika nafasi ya 152, Uganda 161, Rwanda 167, Ethiopia 173 na Burundi 178.

No comments: