Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeitaka Mamlaka
ya Ndani ya Palestina kukomesha hujuma zake dhidi ya wananchi wasio na
hatia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Afisa wa ngazi za juu
katika ofisi ya kisiasa ya HAMAS, Saleh al-Aruri amesema hatua ya vyombo
vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kuwakamata raia wasio
na hatia pamoja na kuwazuia shakhsia wa kisiasa ni jambo lisilokubalika
na kwamba ni ukiukaji wa makubaliano ya huko nyuma kati ya makundi ya
Fat'h na Hamas.
Aruri amesema kuendelea kukamatwa wanamapambano wa
makundi ya muqawama ya Palestina kutaathiri makubaliano ya umoja wa
kitaifa na hivyo kuzidi kumpa adui Mzayuni nguvu ya kuwagawa
Wapalestina. Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita, Mamlaka
ya Ndani ya Palestina ilitangaza kuwakamata wapiganaji kadhaa wa makundi
ya muqawama ya Palestina baada ya msako mkali katika miji kadhaa
inayodhibitiwa na mamlaka hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment