Hali ya kiafya ya shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi
nchini Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela imeendelea kuwa tata na
inasemekana kuwa ndugu na jamaa wa mwanasiasa huyo mkongwe hawana
matumaini tena na kupona kwake.
Mwana wa kike wa Nelson Mandela, Makaziwe Mandela, amewaambia
waandishi habari mjini Pretoria kwamba hali ya baba yake ni mbaya na
kwamba kila kitu kinaweza kutokea. "Hali ya baba ni mbaya sana na kila
kitu kinaweza kutokea, ingawa Mwenyezi Mungu ndiye anayejua wakati wa
kuondoka", amesisitiza Makaziwe.
Hali mbaya ya kiafya ya Mzee Nelson Mandela imemlazimisha Rais Jacob
Zuma kuvunja safari yake nje ya nchi. Hii ni mara ya kwanza kwa Rais
Zuma kusitisha shughuli zake za umma tangu Mandela alazwe hospitalini
mapema mwezi huu.
Wakati huo huo idadi kubwa ya watu imeendelea kukusanyika mbele ya
hospitali ya matibabu ya moyo mjini Pretoria wakimuombea dua shujaa wa
nchi yao.
No comments:
Post a Comment