Serikali ya Pakistan imesema kuwa
inataka kukomeshwa mashambulizi ya ndege za Marekani zisizo na rubani
katika maeneo ya kikabila nchini humo. Sartaj Aziz, Mshauri wa Waziri
Mkuu wa Pakistan katika masuala ya nje na usalama wa taifa ameliambia
bunge la nchi hiyo kuwa sera mpya inabuniwa ili kukomesha mashambulizi
ya ndege za Marekani zisizo na rubani nchini humo.
Aziz ameongeza kuwa serikali imeeleza
wasiwasi wake kwa Washington kutokana na mashambulizi hayo na kwamba
Islamabad inayachukulia mashambulizi hayo ya Marekani kuwa ni ukiukaji
wa mamlaka na kujitawala nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment