Ruud Lubbers, waziri mkuu wa zamani wa Uholanzi ameeleza kuwa mabomu ya
nyuklia 22 ya Marekani yamehifadhiwa katika kituo cha jeshi la anga
nchini humo. Lubbers amethibitisha kuwa mabomu hayo ya nyuklia ya
Marekani yamekuwa yakihifadhiwa katika vyumba imara chini ya ardhi huko
kwenye kituo cha kijeshi cha jeshi la anga cha Brabant. Ruud Lubbers
aliyekuwa waziri mkuu wa Uholanzi kuanzia mwaka 1982 hadi 1984 ni afisa
wa kwanza wa ngazi ya juu wa Uholanzi kukiri kuweko mabomu ya nyuklia
katika ardhi ya nchi hiyo. Mabomu hayo ya nyuklia ya Marekani yametajwa
kuwa ni aina ya B61 yaliyozalishwa nchini Marekani katika muongo wa 60
na kwamba yana nguvu mara nne zaidi ya yale yaliyotumiwa katika miji ya
Japan ya Hiroshima na Nagasaki wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment