Rais Macky Sall wa Senegal amesema nchi yake haiko tayari
kuruhusu ushoga na maingiliano ya ngono kati ya watu wenye jinsia moja.
Sall aliyasema hayo jana akijibu matamshi ya mgeni wake Rais Barack
Obama wa Marekani aliyezitaka nchi za Kiafrika ziwape mashoga
alichokiita haki sawa na makundi mengine ya kijamii. Rais Macky Sall
amemjibu Obama akisema: Japo Senegal imeonyesha ustahamilivu mkubwa
lakini haiko tayari kuruhusu maingiliano ya ngono kati ya watu wenye
jinsia moja.
Obama alikuwa amezitaka nchi za Afrika kuwapa mabaradhuli haki sawa
na makundi mengine ya kijamii bila ya kujali mbari, dini na jinsia zao.
Nchi nyingi za Afrika zinatambua maingiliano ya kingono kati ya watu wenye jinsia moja kuwa ni kosa la jinai.
katika miaka ya hivi karibuni nchi kama Burundi na Sudan Kusini
zimepasisha sheria zinaotambua maingiliano kama hayo kuwa ni kosa la
jinai na nchi kama Uganda, Nigeria na Liberia zinafanya mikakati ya
kupasisha sheria zinazozidisha adhabu kwa wale wanaofanya vitendo hivyo
vichafu.
No comments:
Post a Comment