Paul Barril afisa wa zamani wa usalama wa Ufaransa amekanusha kuhusika kwenye mauaji ya halaiki ya nchini Rwanda.
Hayo yameelezwa katika hali ambayo, taasisi tatu zisizo wa kiserikali
zimefungua mashtaka mahakamani zikimtuhumu afisa huyo wa Ufaransa kwa
kuhusika kwenye mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Paul Barril mwenye umri wa miaka 67 hivi karibuni alishindwa kufika
kwenye mahakama ya Marseille kutokana na hali mbaya ya kiafya, ili
kujibu tuhuma za kushirikiana na genge kubwa la uhalifu nchini humo.
Muungano wa Haki za Binadamu nchini Ufaransa na Shirikisho la Kimataifa
la Muungano wa Haki za Binadamu yanamtuhumu Barril kwa kutia saini
mkataba wa msaada wa kijeshi na serikali ya Rwanda wakati wa kufanyika
mauaji ya kimbari nchini humo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, katika kipindi cha siku 100 zaidi ya watu
800,000 waliuawa kwenye mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Wahutu wenye
misimamo mikali dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani.
No comments:
Post a Comment