Utawala wa Kizayuni wa Israel unatoa huduma za tiba kwa wapiganaji wa
makundi ya kigaidi nchini Syria. Taarifa zinasema kuwa, mamia ya
magaidi hao ambao wamejeruhiwa kwenye mapigano dhidi ya majeshi ya Syria
wanahamishiwa kwenye hospitali za Israel kwa minajili ya kupata huduma
za tiba. Taarifa hizo zinasema kuwa, tokea mwezi Februari mwaka huu,
madaktari na wafanyakazi wa hospitali za Israel wamepewa amri na
makamanada wa jeshi la utawala huo kutoa huduma kwa majeruhi
wanaopelekwa kwenye hospitali za utawala huo ghasibu.
Hii ni katika hali
ambayo, uingiliaji wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, pamoja na nchi za
eneo kama vile Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala wa Kizayuni wa
Israel kwenye mgogoro wa Syria, umesababisha mgogoro wa nchi hiyo
kushadidi na kuwa tata zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment