Watu 22 wameuliwa katika mashambulio
tafauti yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram kaskazini
mashariki mwa Nigeria. Mashambulizi hayo yaliwalenga wanafunzi na wavuvi
huko Maiduguri makao makuu na mji mkubwa zaidi katika jimbo la Borno.
Duru moja ya kijeshi nchini Nigeria imeripoti kuwa wanamgambo wa Boko
Haram waliishambulia shule moja ya binafsi huko Jajeri katika vitongoji
vya Maiduguri na kuwafyatulia risasi wanafunzi waliokuwa wakifanya
mtihani wa taifa.
Wanafunzi tisa waliuliwa papo hapo huku
wengine wengi wakijeruhiwa. Mbali na wanafunzi hao, wanamgambo wa kundi
la Boko Haram waliwaua pia wavuvi 13 na wachuuzi wa chai huko katika
eneo la mto Alau hapo jana.
No comments:
Post a Comment