Milipuko kadhaa ya mabomu iliyowalenga mashabiki wa soka
imetikisa mikahawa kadhaa mjini Baghdad na viunga vyake na kuua watu
wasiopungua 22.
Huko kusini mwa Baghdad mabomu mawili yamelipuka katima mkahawa na
kuua watu 8 waliokuwa wakitazama mpira na kujeruhi wengine kadhaa.
Milipuko mengine miwili ya mabomu imetokea Baquba, kilimita 50 kutoka
mjini Baghdad na kuu mashabiki 10 wa mpira wa miguu.
Milipuko mingine kama hiyo imetokea katika maeneo ya Iskandariya na Jbela.
Duru za hospitali na polisi ya Iraq zinasema kwa ujumla watu
wasiopungua 22 waliawa jana katika mfululizo wa milipuko hiyo na makumi
ya wengine kujeruhiwa.
Zaidi ya watu 2000 wameuawa katika maeneo mbalimbali ya Iraq tangu
mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu pekee katika mfululizo wa mabumu
yanayosadikwia kutengwa na makundi ya kisalafi na kiwahabi yanayoungwa
mkono na kufadhiliwa na baadhi ya nchi za Kiarabu kama Saudi Arabia na
Qatar.
No comments:
Post a Comment