Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa, mapigano yaliyotokea huko mashariki mwa nchi hiyo yamepelekea kuuawa watu 25 nchini humo. Habari zinasema kuwa, watu hao 25 waliouawa wanatoka katika kundi la askari waliojitenga na jeshi la nchi hiyo wanaoongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda. Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende amesema kuwa, watu hao waliuawa walipokuwa wakijaribu kuushambulia mji wa Bunagana unaopatikana mkoani Kivu Kaskazini nchini humo. Mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa nchi hiyo yameongezeka katika siku za hivi karibuni. Mapigano hayo yamepelekea maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao na kuelekea nchi jirani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment