Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 22, 2012

FAO yaonya kuwepo hali mbaya katika nchi za eneo la Sahel la Afrika

Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo FAO limezionya nchi za eneo la Sahel la Afrika kutokana na hali mbaya inayowakabili wananchi wa nchi hizo. Shirika hilo limezitaka nchi za eneo la Sahel kupunguza sababu zinazopelekea kuongezeka uhaba wa chakula katika nchi hizo. FAO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR kwa pamoja yametangaza kuunda mikakati ya kukusanya chakula kwa ajili ya malaki ya watu wa nchi za Afrika hususan Mali ambao wamekimbilia nchi jirani kufuatia machafuko ya kivita nchini kwao. Aidha Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo limetangaza kuwa, mpango huo utatumika katika nchi za eneo la Sahel sambamba na kukabiliana na lishe duni inayowakabili watu milioni tatu na nusu katika eneo hilo. Mapigano ya hivi karibuni nchini Mali yamepelekea maelfu ya wananchi wa nchi hiyo kuwa wakimbizi, na kusababisha eneo la Sahel kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

No comments: